FAHAMU AFYA YA TEZI DUME - PROSTATE GLAND
Kila mwanaume anazaliwa na Tezi dume. Tezi dume siyo ugonjwa bali ni kiungo kama viungo vingine mwilini. Tezi dume inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa nikutengeneza majimaji ya uzazi wa mwanaume (shahawa), ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizo tengenezwa kutoka kwenye Korodani; na husaidia mbegu za kiume kubaki hai kwa muda unaostahili. Tatizo linakuja kiungo hiki kinapoanza kutanuka. Kiungo hiki kinatanuka taratibu taratibu mnoo. Hili ni tatizo linalo wakumba wanaume wengi. Takwimu zinaonesha kwamba kati ya wanaume 10, wa 5 na kuendelea wana dalili za kutanuka kwa Tezi dume . Ukuwaji wa Tezi dume ni ile hali ya chembe chembe hai katika tezi ya kiume kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili katika eneo linalo zunguka mirija ya kupitisha mkojo na mbegu za kiume. Tatizo hili kwa sasa linawapata wanaume kuanzia umri wa miaka 25 na kuendelea, tofauti na awali lilikuwa miaka zaidi ya 50.