Posts

Showing posts from February, 2018

UFAHAMU KUHUSU HOMA YA INI

Image
Inakadiliwa kwamba  zaidi ya watu milioni 350 wanaishi na virus vya ugonjwa wa ini Duniani. Takwimu Za  mwaka 2015 zinaonesha kwamba zaidi ya watu 900,000 walifariki kutokana na ugonjwa huu wa homa  ya ini. Lakini pia licha ya kuwa ugonjwa huu unaua mamilioni ya watu Kila mwaka. Ugonjwa huu huwa hauna dalili zile Za moja kwa moja Na kipekee zenye  kumwonesha mtu Kama ameathirika na ugonjwa huu. Hivyo Basi ,Homa ya Ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya virusi ambayo ikishaingia mwilini hushambulia Ini. Kabla ya kugeuka maradhi sugu.Virusi hivi vinaitwa HBV (Hepatitis B Virus) .Virus hivi husambazwa kwa njia ya damu, majimaji, mate au jasho. Ugonjwa huu usipochukuliwa hatua mapema husababisha vimbe Na kupelekea kifo. Virus hivyo vya homa ya ini  huweza kuishi kwa muda mrefu zaidi nje ya mwili Na huweza kumuambukiza mtu bila kujua.Na inakadiliwa  virus  hivi kuwa ni hatari zaidi ya virus ya UKIMWI. JINSI INAVYOAMBUKIZWA : Katika maeneo hatari zaidi d