UFAHAMU KUHUSU HOMA YA INI







Inakadiliwa kwamba  zaidi ya watu milioni 350 wanaishi na virus vya ugonjwa wa ini Duniani. Takwimu Za  mwaka 2015 zinaonesha kwamba zaidi ya watu 900,000 walifariki kutokana na ugonjwa huu wa homa  ya ini. Lakini pia licha ya kuwa ugonjwa huu unaua mamilioni ya watu Kila mwaka.
Ugonjwa huu huwa hauna dalili zile Za moja kwa moja Na kipekee zenye  kumwonesha mtu Kama ameathirika na ugonjwa huu.

Hivyo Basi ,Homa ya Ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya virusi ambayo ikishaingia mwilini hushambulia Ini. Kabla ya kugeuka maradhi sugu.Virusi hivi vinaitwa HBV (Hepatitis B Virus) .Virus hivi husambazwa kwa njia ya damu, majimaji, mate au jasho. Ugonjwa huu usipochukuliwa hatua mapema husababisha vimbe Na kupelekea kifo.

Virus hivyo vya homa ya ini  huweza kuishi kwa muda mrefu zaidi nje ya mwili Na huweza kumuambukiza mtu bila kujua.Na inakadiliwa  virus  hivi kuwa ni hatari zaidi ya virus ya UKIMWI.

JINSI INAVYOAMBUKIZWA:

Katika maeneo hatari zaidi duniani, Virusi vya Hepatitis B (HBV) kwa kawaida husambazwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa au kutoka kwa mtu mmoja  kwenda mwingine kama  ilivyo kwa Ukimwi.Virusi vya Homa ya Ini pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, mate, jasho na mwingiliano wowote ule wa damu.

Zipo njia  mbalimbali ambazo hupelekea maambukizi ya homa ya Ini ni Kama vile;

1. Kujamiana bila kinga
2. Kunyonyana ndimi 'denda'
3. Mama mwenye ugonjwa humwambukiza  mtoto wakati wa kujifungua
4. Kuchangia damu isiyo salama
5. Kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
6. Kuchangia miswaki
7. kuchangia taulo na mwenye ugonjwa huo
8. Kubadilishana nguo au kukumbatiana wakati mkiwa mnavuja jasho.




Tafiti za kitaalamu zinaonesha kuwa virusi hivyo hivyo huweza kuishi nje ya mwili. Vinaweza kuishi  kwa muda mrefu zaidi  yaani siku saba. Lakini virusi vya UKIMWI,havina  uwezo wa kuishi nje ya mfumo wa damu hata kwa dakika moja.
Kutokana na usugu wa HBV  kama kirusi kipo kwenye ngozi, kitaendelea kuwa hai kwa siku saba na katika kipindi hicho mtu anaweza kuambukizwa kwa njia ya damu au jasho.

Kwa wastani kirusi cha HBV kikishaingia mwilini, hupevuka ndani ya siku 75, hata hivyo upo uwezekano wa kupevuka kati ya siku 30 hadi 180. Ndani ya siku 30 mpaka 60, mtu mwenye homa ya Ini anaweza kugundulika ikiwa atapimwa.

Mtu mwenye Homa ya Ini ana wastani mdogo wa kuishi kuliko maambukizi ya virusi vya UKIMWI.Kwa maana hiyo, mwenye maambukizi ya Virusi vya Homa ya Ini hufariki dunia haraka kuliko mwenye VVU.


DALILI ZA UGONJWA HUU:

Watu wengi hawaonyeshi dalili yoyote. Kwa maana hiyo mtu anaweza kuishi na HBV na kusababisha maambukizi kwa wengine bila kugundulika.

Dalili hizo ni:
1. Uchovu
2. Kichefuchefu
3. Mwili kuwa dhaifu
4. Homa kali
5. Kupoteza hamu ya kula
6. Kupungua uzito
7. Maumivu makali ya tumbo upande wa ini
8. Macho na ngozi kuwa vya njano
9. Mkojo mweusi
10. Saratani ya Ini





Kundi lipi ni Hatari zaidi;

Asilimia 80-90 ya watoto wachanga ambao huambukizwa katika kipindi cha mwaka wa kwanza tangu kuzaliwa, Homa ya Ini hukua mpaka kufikia kuwa sugu na hatimaye kifo.

Asilimia 15-25 ya watu wazima ambao  walipata utotoni na hatimaye Hepatitis B  kuwa sugu,kufariki dunia kutokana na matokeo ya Ini  kuharibika kabisa na  kuwa saratani ya Ini.

MADHARA YA HOMA YA INI
1.Kukosa choo
2.Mwili kudhoofika
3.Kupungua kwa kinga ya mwili.
4.Kifo.

Virusi  ya homa ya Ini huathiri  mfumo mzima wa mwili, hali ambayo hupelekea organi mbalimbali za mwili kushindwa kufanya kazi vyema. Organi mbalimbali Kama vile moyo,figo,kongosho nk.hushindwa kufanya kazi nzuri na hatimaye kinga ya mwili kushuka na kupelekea kifo.


SULUHISHO
Hakuna tiba ya moja kwa moja ya ugonjwa huu wa homa ya Ini. Lakini kuna njia bora na asili za kuboresha kinga ya mwili  na kupunguza  athari za kuukuza ugonjwa huu kuwa mkubwa zaidi yaani saratani au athari zake kuwa kubwa zaidi.

Suluhisho la  kudumu
Vipo virutubisho ambavyo husaidia katika kupunguza makali ya ugonjwa huu.

Faida ya virutubisho hivi kwa mtumiaji :
1. Husaidia katika kuua bacteria na virusi nyemelezi ambao huathiri Ini.
2. Husaidia katika kuboresha na kuimairisha kinga ya mwili.
3. Husaidia katika kuondoa maumivu ya uchovu wa mara kwa mara.
4. Husaidia katika kurudisha ubora wa seli za  mwili kuboresha utendaji kazi wa seli za mwili.
5. Husaidia katika kuongeza nguvu na ,kuboresha mmeng’enyo wa Chakula 
6. Husaidia kupunguza kiwango cha mafuta ambayo hupelekea saratani.      
7. Virutubisho hivi huwa na madini ,vitamin,protini,amino acids na virutubisho  vya kambakamba ambavyo ni muhimu zaidi katika kuimairisha kinga ya mwili.





Kwa uhitaji wa virutubisho vya kuboresha na kuimarisha Afya yake awasiliane na kampuni kwa namba ifuatavyo:-

                                                     








Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU AFYA YA TEZI DUME - PROSTATE GLAND

UFAHAMU JUU YA MVURUGIKO WA HOMONI KWA MWANAMKE

UFAHAMU WA KINA KUHUSU TATIZO LA BAWASIRI.