UFAHAMU KUHUSU HOMA YA INI
Inakadiliwa kwamba zaidi ya watu milioni 350 wanaishi na virus vya ugonjwa wa ini Duniani. Takwimu Za mwaka 2015 zinaonesha kwamba zaidi ya watu 900,000 walifariki kutokana na ugonjwa huu wa homa ya ini. Lakini pia licha ya kuwa ugonjwa huu unaua mamilioni ya watu Kila mwaka. Ugonjwa huu huwa hauna dalili zile Za moja kwa moja Na kipekee zenye kumwonesha mtu Kama ameathirika na ugonjwa huu. Hivyo Basi ,Homa ya Ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya virusi ambayo ikishaingia mwilini hushambulia Ini. Kabla ya kugeuka maradhi sugu.Virusi hivi vinaitwa HBV (Hepatitis B Virus) .Virus hivi husambazwa kwa njia ya damu, majimaji, mate au jasho. Ugonjwa huu usipochukuliwa hatua mapema husababisha vimbe Na kupelekea kifo. Virus hivyo vya homa ya ini huweza kuishi kwa muda mrefu zaidi nje ya mwili Na huweza kumuambukiza mtu bila kujua.Na inakadiliwa virus hivi kuwa ni hatari zaidi ya virus ya UKIMWI. JINSI INAVYOAMBUKIZWA ...