UFAHAMU JUU YA MVURUGIKO WA HOMONI KWA MWANAMKE
Mvurugiko wa homoni za mwanamke ni kitendo cha kuongezeka au kupungua kwa vichochezi katika mwili wa mwanamke pale anapo pata hedhi, hivyo kufanya mwili kubadilika. Mvurugiko huo huathiri kila mwanamke kwa zaidi ya 80%. Asilimia kubwa ya wanawake mabadiliko huanza kati ya miaka 40 na 50, lakini pia kukosekana kwa usawa wa homoni huweza kuonekana mapema zaidi, kuanzia miaka 14. Mabadiliko haya asilia hutokea wakati wa balehe, hedhi, ujauzito, kabla na baada ya ukomo wa hedhi. Mvurugiko wa homoni kwa mwanamke huweza kuchangiwa kutokuwepo na usawa katika homoni zifuatazo Estrogen, Progesterone na Testosterone. Kupungua au kuzidi kwa homoni hizi hupelekea mvurugiko wa homoni kwa mwanamke. ...